La kusema pindi watu wanataka kukudhuru

Inatakikana kwa mtu ambaye watu wamemkusanyikia au wanamfanyia uadui aseme:

حَسْبُنَا اللّهُ وَنِعْمَ الْوَكِيلُ

“Allaah pekee anatutosheleza na Yeye ndiye mbora wa kutegemewa.

Akisema hivi basi Allaah atamtosheleza na shari yao kama jinsi alivyomtosheleza Ibraahiym na Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhimaa wa sallam). Liweke neno hili siku zote kichwani. Ukiona watu wanataka kukufanyia uadui useme:

حَسْبُنَا اللّهُ وَنِعْمَ الْوَكِيلُ

“Allaah pekee anatutosheleza na Yeye ndiye mbora wa kutegemewa.”

Allaah (´Azza wa Jall) atakutosheleza na shari yao.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Riyaadh-is-Swaalihiyn (01/557)
  • Imechapishwa: 25/07/2023