272. Ni ipi hukumu ya wanawake kuyatembelea makaburi?

Swali 272: Ni ipi hukumu ya wanawake kuyatembelea makaburi?

Jibu: Ni haramu na dhambi kubwa wanawake kuyatembelea makaburi. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amewalaani wanawake wenye kuyatembelea makaburi. Lakini mwanamke akipita kando na makaburi pasi na kukusudia matembezi, basi hapana neno kusimama na akawaombea du´aa wale wafu. Hivo ndivo inavyoashiria Hadiyth[1] ya ´Aaishah katika “as-Swahiyh” ya Muslim.

[1] Muslim (974).

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (17/313)
  • Imechapishwa: 29/05/2022