1 – Ni lazima maiti kumzika ndani ya kaburi ili kumlinda kutokamana na wanyama wakali. Maiti anatakiwa kuelekezwa Qiblah. Kila ambavo kaburi litakuwa na kina ndio bora zaidi.

2 –  Bora kaburi liwe na mwanandani. Mwanandani atachimbwa upande wa Qiblah na humo ndipo atawekwa maiti.

3 – Inafaa kuchimba mwanandani katikati ya kaburi[1] haja ikipelekea kufanya hivo.

4 – Maiti atalazwa ubavuni mwake wa kulia hali ya kuelekezwa Qiblah.

5 – Matofali ya block na matofali ya udongo yanatakiwa kumtenganisha na kaburi ili udongo usimdondokee maiti.

6 – Mwishowe kaburi litafukiwa tena. Haitakiwi kunyanyuliwa, lisitiwe chokaa wala kitu kingine.

7 – Haijuzu kuzika katika nyakati tatu:

1 – Jua likichomoza mpaka lipande kiasi cha takriban robo saa.

2 – Kipindi ambapo jua limepinduka mpaka liache kilele chake. Bi maana tariban dakika saba baada yake.

3 – Kukibaki takriban robo saa kabla ya jua kuzama mpaka lizame.

Imeandikwa na Muhammad bin Swaalih al-´Uthaymiyn

1402-02-02

Himdi zote ni stahiki ya Allaah, Mola wa walimwengu.

[1] Tazama https://firqatunnajia.com/95-aina-mbili-za-mianandani-ambazo-zote-zinafaa/#_ftn2

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (17/475-476)
  • Imechapishwa: 28/05/2022