274. Inafaa kwa mwanamke kulitembelea kaburi la Mtume?

Swali 274: Ni ipi hukumu kwa wanawake kulitembelea kaburi la Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)?

Jibu: Ni haramu kwa mwanamke kuyatembelea makaburi kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amewalaani wanawake wanaoyatembelea makaburi. Laana ni kule kuwekwa mbali na rehema za Allaah. Laana haiwi juu ya kitendo isipokuwa inapokuwa ni dhambi kubwa. Kwa ajili hiyo wanazuoni wamesema kuwa kila dhambi ambayo adhabu yake imefanywa ni kulaaniwa basi ni miongoni mwa madhambi makubwa.

Kuhusu wanawake kulitembelea kaburi la Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), wako baadhi ya wanazuoni wenye kuona hakuna vibaya kwa sababu ukweli wa mambo sio kulitembelea kaburi kwa kuwa limezungukwa na kuta zinazoitenganisha. Hata kama atasimama karibu nalo kulitembelea ukweli wa mambo ni kwamba hakulitembelea kaburi. Kwa sababu limezungushiwa kuta tatu, kama alivosema Ibn-ul-Qayyim. Kwa ajili hiyo baadhi ya wanazuoni wakabagua matembezi haya na wakasema kuwa ukweli wa mambo sio matembezi kwa kuwa mwanamke halitembelei kaburi moja kwa moja. Lakini tahadhari zaidi ni yeye kutofanya hivo. Tunamshauri mwanamke ajifanyie wepesi. Anaposema:

السلام عليك أيها النبي و رحمة الله و بركاته

“Amani, rehema na baraka za Allaah ziwe juu yako, ee Mtume!”

basi utambue kuwa wako Malaika wanaomfikisha salamu hii Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Niswalieni sana. Kwani hakika salamu zenu naonyeshwa.”[1]

Akiwa mbali na kaburi umbali anaoweza kuwa basi salamu yake inamfikia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Kwa hiyo ajifanyie wepesi nafsi yake. Atambue kuwa hayamzuilii mambo ya kheri. Anaweza vilevile kulitembelea bustani ambalo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema juu yake:

“Kati ya nyumba yangu na mimbari yangu ni bustani miongoni mwa mabustani ya Peponi.”[2]

Hili limeenea kwa wanamme na wanawake.

[1] Abu Daawuud (1047).

[2] al-Bukhaariy (1195) na Muslim (1390).

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (17/315-316)
  • Imechapishwa: 29/05/2022