24. Hadiyth “Kitu cha kwanza ambacho mja atafanyiwa hesabu kwacho… “

376 – ´Abdullaah bin Qurt (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

أولُ ما يحاسب به العبدُ يومَ القيامةِ الصلاةُ، فإنْ صَلَحَتْ؛ صَلَحَ سائرُ عَملِه، وإنْ فسدتْ؛ فَسَدَ سائرُ عملِه

“Kitu cha kwanza ambacho mja atafanyiwa hesabu kwacho siku ya Qiyaamah ni swalah. Ikiwa vizuri, basi yatakuwa vizuri matendo yake yaliyosalia, na ikiharibika, basi yataharibika matendo yake yaliyosalia.”[1]

Ameipokea at-Twabaraaniy katika “al-Mu´jam al-Awsatw” kwa cheni ya wapokezi isiyokuwa na neno –  Allaah akitaka.

[1] Swahiyh kupitia zingine.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Adhwiym bin ´Abdil-Qawiy al-Mundhiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/274)
  • Imechapishwa: 15/11/2023
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy