Imaam an-Nawawiy (Rahimahu Allaah) amesema:

عن أبي هريرة رضي الله عنه أنَّ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم قَالَ: (حُجِبَتِ النَّارُ بالشَّهَواتِ، وَحُجِبَتِ الجَنَّةُ بِالمَكَارِهِ). مُتَّفَقٌ عَلَيه

101 – Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Moto umezungukwa na matamanio. Pepo imezungukwa na mambo yenye kuchukiza.”

al-Bukhaariy na Muslim

Moto umezungukwa na matamanio. Pepo imezungukwa na mambo yenye kuchukiza. Hivyo basi, pambana na nafsi yako juu ya yale anayoyapenda Allaah hata kama utayachukia. Tambua ya kwamba ikiwa utailazimisha nafsi yako kwa kumtii Allaah, mwishowe utakuja kupenda kumuabudu Allaah. Itafikia wakati ambapo baada ya kuwa moyo wako ulikuwa unachukia utakukatalia endapo utataka kufanya maasi. Hebu jaribu hili uone.

Tunaona baadhi ya watu  wanachukia kuswali na mkusanyiko na hilo linamkuia zito kwake pale anapoanza kulitendea kazi. Lakini baadaye kuswali na mkusanyiko inakuwa ni burudisho kwake.

Hivyo basi, izoweze nafsi yako. Mwanzoni utachukia. Lakini hata hivyo baadaye itakuja kukuwia sahali na kulinyenyekea.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Riyaadh-is-Swaalihiyn (02/91)
  • Imechapishwa: 15/11/2023