22. Yanayofaa kwa mfungaji: Maji kuingia kooni kwa bahati mbaya

2 – Mwenye kuoga, kusukutua au alikuwa akipandisha maji kwenye pua na maji yakaingia kooni mwake bila kukusudia swawm yake haiharibiki. Kadhalika yule ambaye nzi itaruka na kuingia kooni mwake, vumbi barabarani, unga wa ngano na mfano wa hivo haviharibu swawm yake kwa kutokuweza kujiepusha navyo. Jengine ni kwa sababu hakukusudia, hakutaka wala hakuchagua mwenyewe. Allaah (Ta´ala) amesema:

لَا يُكَلِّفُ اللَّـهُ نَفْسًا إِلَّا وُسْعَهَا

”Allaah hakalifishi nafsi yoyote isipokuwa kwa kadiri ya uwezo wake.”[1]

[1] 02:286

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Duruus fiy Ramadhwaan, uk. 42-43
  • Imechapishwa: 19/04/2023