3 – Inafaa kwa mfungaji kuchelewesha kuoga josho la janaba baada ya kupambazuka alfajiri. Imethibiti kwa al-Bukhaariy na Muslim waliopokea kupitia kwa ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa) ambaye amesimulia:
“Alfajiri ilikuwa ikimkuta naye yuko na janaba kutoka kwa mkewe. Kisha anaoga na kufunga.”[1]
[1] al-Bukhaariy (1926) na Muslim (1109).
- Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Duruus fiy Ramadhwaan, uk. 43
- Imechapishwa: 19/04/2023