Himdi zote njema anastahiki Allaah. Swalah na amani zimwendee Mtume wa Allaah, kizazi chake na Maswahabah zake wote.

Ama baada ya hayo;

Miongoni mwa wepesi wa Shari´ah ni zile ruhusa zilizokuja za swawm. Miongoni mwazo:

1 – Mwenye kula au kunywa kwa kusahau basi funga yake ni sahihi. Hatolazimika kulipa kwa mujibu wa maoni sahihi zaidi ya wanazuoni. Imethibiti kwa al-Bukhaariy na Muslim waliopokea kupitia kwa Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) ambaye amesimulia kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Akisahau ambapo akala na kunywa, basi akamilishe funga yake. Hakika hapana vyenginevyo Allaah ndiye kamilisha na kumnywesha.”[1]

Tamko la Muslim linasema:

“Mwenye kusahau hali ya kuwa amefunga ambapo akala na kunywa, basi akamilishe swawm yake. Hakika si vyenginevyo Allaah ndiye kamlisha na kumnywesha.”[2]

Yale yaliyofahamishwa na Hadiyth kwamba aliyesahau sio wajibu kwake kulipa ndio maoni ya sawa ambayo wameenda kwayo kikosi cha wanazuoni wengi.

[1] al-Bukhaariy (1933) na Muslim (1155).

[2] Muslim (1155).

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Duruus fiy Ramadhwaan, uk. 42
  • Imechapishwa: 19/04/2023