20. Dalili za kupendeza kuharakisha kufungua na kuchelewesha daku

Miongoni mwa dalili zinazofahamisha kupendeza kuharakisha kukata swawm:

1 – Imethibiti kwa al-Bukhaariy na Muslim waliopokea kupitia kwa ´Umar  bin al-Khattwaab (Radhiya Allaahu ´anh) ambaye amesimulia kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Usiku ukija hapa [mashariki] na ukaondoka mchana hapa [magharibi] na likazama jua, basi amekwishafungua mfungaji.”[1]

2 – Kuchelewesha daku. Allaah (Ta´ala) amesema:

وَكُلُوا وَاشْرَبُوا حَتَّىٰ يَتَبَيَّنَ لَكُمُ الْخَيْطُ الْأَبْيَضُ مِنَ الْخَيْطِ الْأَسْوَدِ مِنَ الْفَجْرِ اللَّيْلِ

“Kuleni na kunyweni mpaka ubainike kwenu weupe wa alfajiri katika weusi wa usiku.”[2]

Vilevile imethibiti kwa al-Bukhaariy na Muslim waliopokea kupitia kwa Ibn ´Umar (Radhiya Allaahu ´anhumaa) ambaye amesimulia kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Hakika Bilaal anaadhini usiku. Hivyo kuleni na kunyweni mpaka aadhini Ibn Umm Maktuum.”

al-Qaasim bin Muhammad – mmoja katika wasimuliaji wa Hadiyth hiyo – amesema:

“Kitambo kilichokuwepo kati yake [daku na adhaana] ni kupanda kwa huyu na kushuka kwa huyu.”[3]

Miongoni mwa dalili zinazofahamisha kupendeza kwa daku ni yale yaliyothibiti kwa al-Bukhaariy na Muslim waliopokea kupitia kwa Anas (Radhiya Allaahu ´anh) ambaye ameeleza kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Kuleni daku. Kwani hakika katika kula daku kuna baraka.”[4]

3 – Inapendeza kuchelewesha daku kutokana na yaliyothibiti kwa al-Bukhaariy na Muslim waliopokea kupitia kwa Yaziyd bin Thaabit (Radhiya Allaahu ´anh) ambaye amesimulia:

“Tulikula daku pamoja na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kisha akasimama kuswali.”Nikauliza: “Kulikuwa na kitambo gani kati ya adhaana na daku?”Akasema: “Kiasi cha Aayah khamsini.”[5]

Allaah awawafikishe wote kumtii, awaruzuku wote elimu yenye manufaa na matendo mema.

Swalah na amani zimwendee Mtume wa Allaah, kizazi chake na Maswahabah zake wote.

[1] al-Bukhaariy (1954) na Muslim (1100).

[2] 02:187

[3] al-Bukhaariy (617) na Muslim (1092).

[4] al-Bukhaariy (1923) na Muslim (1095).

[5] al-Bukhaariy (1921) na Muslim (1097).

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Duruus fiy Ramadhwaan, uk. 40-41
  • Imechapishwa: 19/04/2023