19. Mapendekezo ya kuharakisha kukata swawm na kuchelewesha daku

Himdi zote njema anastahiki Allaah. Swalah na amani zimwendee Mtume wa Allaah, kizazi chake na Maswahabah zake wote.

Ama baada ya hayo;

Miongoni mwa hukumu zinazohusu swawm wakati wa kufungua na daku:

1 – Inapendeza kuharakisha kufungua pale kunapohakikishwa kuwa jua limezama kwa kuliona au kwa maelezo ya mtu mwaminifu na mwadilifu. Imethibiti kwa al-Bukhaariy na Muslim waliopokea kupitia kwa Sahl (Radhiya Allaahu ´anh) ambaye amesimulia kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Watu hawatoacha kuwa katika kheri muda wa kuwa wanachelewesha kufungua.”[1]

Hilo ni kwa sababu kuharakisha kukata swawm kunajulisha kutekeleza na kuchelewesha kunafahamisha kuchupa mipaka, kama wanavofanya mayahudi na manaswara na baadhi ya mapote yaliyopinda ambao wanachelewesha kufungua mpaka kuchomoza kwa nyota. Imepokelewa katika Sunan ya Abu Daawuud kwamba:

“Mayahudi na manaswara wanachelewesha.”[2]

Ibn Hibbaan ameipokea kwa tamko lisemalo:

“Ummah hautoacha kuwa juu ya Sunnah muda wa kuwa hawasubiri nyota kwa ajili ya kufungua kwao.”[3]

[1] al-Bukhaariy (1957) na Muslim (1097).

[2] Abu Daawuud (2353).

[3] Ibn Hibbaan (3510) na al-Haakim (1574) ambaye amesema:

”Hadiyth hii ni Swahiyh juu ya sharti za al-Bukhaariy na Muslim, ijapo hawakuipokea kwa tamko hili.”

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Duruus fiy Ramadhwaan, uk. 40
  • Imechapishwa: 23/04/2023