22. Hadiyth “Wape bishara njema watembeaji gizani… “

319 – Sahl bin Sa´d as-Saa´idiy (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

لِيُبشرِ المشَاؤون في الظُلَّم إلى المساجدِ بالنورِ التامِّ يومَ القيامةِ

“Wape bishara njema watembeaji gizani kwenda misikitini kupata nuru kamili siku ya Qiyaamah.”[1]

Ameipokea Ibn Maajah, Ibn Khuzaymah katika “as-Swahiyh” ambaye tamko ni lake na pia ameipokea al-Haakim ambaye amesema:

“Ni Swahiyh juu ya sharti za al-Bukhaariy na Muslim.”

Hadiyth hii ameipokea Ibn ´Abbaas, Ibn ´Umar, Abu Sa´iyd al-Khudriy, Zayd bin Haarithah, ´Aaishah na wengineo.

[1] Swahiyh kupitia zingine.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Adhwiym bin ´Abdil-Qawiy al-Mundhiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/247)
  • Imechapishwa: 02/12/2022
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy