23. Hadiyth “Yule mwenye kutoka nyumbani kwake hali ya kuwa amejitwahirisha… “

320 – Abu Umaamah (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

مَن خرجَ من بيتِه متطهِّراً إلى صلاة مكتوبةٍ؛ فأجْرهُ كأجرِ الحاجِّ المُحْرِم، ومَن خرج إلى تَسَبيح الضحى لا يُنْصِبه إلا إياه؛ فأجرُه كأجر المُعْتَمِرِ، وصلاةٌ على أَثَرِ صلاةٍ، لا لَغْوَ بينهما كتابٌ في عِلِّيين

“Yule mwenye kutoka nyumbani kwake hali ya kuwa amejitwahirisha kuiendea swalah ya faradhi, basi ujira wake ni kama wa mwenye kufanya hajj na Ihraam. Na yule mwenye kutoka kwa ajili ya kuswali Dhuhaa na hakuna alichokusudia isipokubwa yenyewe, basi ujira wake ni kama wa mwenye kufanya ´umrah. Swalah baada ya kumalizika swalah nyingine pasi na mazungumzo ya kipuuzi kati yazo, inaandikwa kwa juu kabisa.”[1]

[1] Nzuri.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Adhwiym bin ´Abdil-Qawiy al-Mundhiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/247)
  • Imechapishwa: 02/12/2022
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy