24. Hadiyth “Watu aina tatu wote wamedhaminiwa na Allaah… “

321 – Yeye pia huyohuyo amesimulia kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

ثلاثةٌ كلّهم ضامنٌ على الله إنْ عاش رُزِق وكُفِيَ، وإنْ ماتَ أدخلهُ الله الجنّةَ، مَن دخل بيته فسَلَّم، فهو ضامنٌ على الله، ومن خرج إلى المسجدِ فهو ضامنٌ على الله، ومَن خرجَ في سبيل الله فهو ضامنٌ على الله

“Watu aina tatu wote wamedhaminiwa na Allaah; yule mwenye kuishi, ataruzuku na kutoshelezwa, na mwenye kufa, Allaah atamwingiza Peponi: mwenye kuingia nyumbani kwake akatoa salamu, Allaah ni Mwenye kumdhamini. Na mwenye kutoka kwenda msikitini, Allaah ni Mwenye kumdhamini. Na mwenye kutoka kwenda katika njia ya Allaah, Allaah ni Mwenye kumdhamini.”[1]

Ameipokea Abu Daawuud na Ibn Hibbaan katika “as-Swahiyh” yake.

[1] Swahiyh.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Adhwiym bin ´Abdil-Qawiy al-Mundhiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/248)
  • Imechapishwa: 02/12/2022
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy