25. Hadiyth “Yule ambaye atatawadha nyumbani kwake… “

322 – Salmaan (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

مَن توضّأ في بيته فأحسنَ الوضوءَ، ثم أتى المسجدَ؛ فهو زائرُ الله، وحَقٌّ على المَزور أنْ يُكرمَ الزائرَ

“Yule ambaye atatawadha nyumbani kwake, akaufanya vizuri wudhuu´, kisha akaja msikitini, basi huyo ni mgeni wa Allaah. Ni haki kwa yule mtembelewaji kumkirimu mgeni.”[1]

 Ameipokea at-Twabaraaniy katika “al-Mu´jam al-Kabiyr” kwa cheni mbili ambapo moja wapo ni nzuri.

[1] Nzuri.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Adhwiym bin ´Abdil-Qawiy al-Mundhiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/248)
  • Imechapishwa: 02/12/2022
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy