21. Hadiyth “Yule mwenye kutembea katika giza la usiku kwenda… “

318 – Abud-Dardaa´ (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

مَن مشى في ظلمةِ الليلِ إلى المسجدِ، لَقي الله عز وجل بنورٍ يوم القيامة

“Yule mwenye kutembea katika giza la usiku kwenda msikitini, basi atakutana na Allaah akiwa na nuru siku ya Qiyaamah.”[1]

Ameipokea at-Twabaraaniy katika “al-Mu´jam al-Kabiyr” kwa cheni ya wapokezi nzuri na Ibn Hibbaan katika “as-Swahiyh” kwa tamko lisemalo:

مَن مشى في ظلمةِ الليل إلى المساجد؛ آتاه الله نُوراً يوم القيامةِ

“Yule mwenye kutembea katika giza la usiku kwenda mskitini, basi Allaah (´Azza wa Jall) atamtia nuru siku ya Qiyaamah.”

[1] Swahiyh kupitia zingine.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Adhwiym bin ´Abdil-Qawiy al-Mundhiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/247)
  • Imechapishwa: 02/12/2022
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy