Haafidhw Ibn Hajar al-´Asqalaaniy (Rahimahu Allaah) amesema:

12 – Salmaan bin ´Aamir adh-Dhabbiy (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Atapofuturu mmoja wenu basi afuturu kwa tende. Asipopata, basi afuturu kwa maji, kwani hakika hayo ni yenye kutwahirisha.”[1]

Wameipokea watano. Ameisahihisha Ibn Khuzaymah, Ibn Hibbaan na al-Haakim.

Hadiyth hii ni dalili ya mapendezo ya kukata swawm kwa tende. Anas (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza:

“Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akifuturu kwa tende tosa kabla ya kuswali. Ikiwa hakupata tende tosa basi kwa tende za kawaida, ikiwa hakupata tende za kawaida basi anakunywa funda chache za maji.”[2]

Inafahamisha kwamba bora ni kukata swawm kwa tende tosa ikiwezekana, kwa sababu kwa ni tamu zaidi na yenye manufaa zaidi mwilini. Mtu akikosa tende tosa anakata swawm kwa tende za kawaida. Mtu akikosa tende za kawaida anakata swawm kwa maji. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

”… kwani hakika hayo ni yenye kutwahirisha.”

[1] Ahmad (4/16), Abu Daawuud (2355), an-Nasaa’iy katika “as-Sunan al-Kubraa” (3302), at-Tirmidhiy (657), Ibn Maajah (1699), Ibn Khuzaymah (2067), Ibn Hibbaan (3514) na al-Haakim (1/431).

[2] Abu Daawuud (2356), at-Tirmidhiy (696) na Ahmad (03/164).

  • Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Minhat-ul-´Allaam fiy Sharh Buluugh-il-Maraam (05/31)
  • Imechapishwa: 09/02/2025