31. Je, inafaa kwa mwanamke kumswalia maiti?

Swali 31: Je, inafaa kwa mwanamke kuswalia jeneza[1]?

Jibu: Kuswalia jeneza ni jambo lililosuniwa kwa watu wote; wanamme na wanawake. Jeneza linaswaliwa nyumbani au msikitini. Yote hayo ni sawa. ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa) na wanawake wengine walimswalia Sa´d bin Abiy Waqqaas (Radhiya Allaahu ´anh) pindi alipokufa katika msikiti wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Kinacholengwa ni kwamba kuswalia jeneza ni jambo lilolowekwa katika Shari´ah kwa wote. Walichokatazwa ni wao kuyatembelea makaburi na kusindikiza jeneza. Kuhusu kumswalia kwao maiti nyumbani, msikitini, Muswallaa au katika nyumba ya familia yake hapana vibaya kufanya hivo. Wanawake walikuwa wakiswalia jeneza nyuma ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na nyuma ya makhaliyfah waongofu.

[1] Majmuu´-ul-Fataawaa (13/133).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahkaam-ul-Janaa-iz, uk.
  • Imechapishwa: 18/12/2021