32. Thawabu mfano wa mlima wa Uhud kwa atakayemswalia maiti

Swali 32: Kuna mtu ameswalia majeneza matano swalah moja. Je, anapata Qiraatw kwa kila jeneza au Qiraatw inakuwa juu ya idadi ya swalah[1]?

Jibu: Tunataraji amepata Qawaaritw juu ya idadi ya majeneza. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Yeyote atakayeswalia jeneza basi anapata Qiraatw na yeyote atakayelisindikiza mpaka akazikwa basi anapata Qiraatw mbili.”

Zipo Hadiyth nyenginezo zilizopokelewa zikiwa na maana kama hiyo. Zote zinafahamisha kwamba Qawaaritw zinakuwa nyingi kutegemea na idadi ya majeneza. Yule ambaye ataswalia jeneza basi anapata Qiraatw. Yule ambaye atamsindikiza mpaka akazikwa basi anapata Qiraatw. Ambaye atamswalia na akamsindikiza mpaka wakamaliza kuzika anapata basi anapata Qiraatw mbili. Haya ni katika fadhilah za Allaah (Subhaanah), utoaji na ukarimu Wake juu ya waja Wake. Himdi na shukurani zote njema zinarejea Kwake. Hapana mwabudiwa wala mola wa haki mwengine asiyekuwa Yeye.

[1] Majmuu´-ul-Fataawaa (13/136-137).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahkaam-ul-Janaa-iz, uk. 28
  • Imechapishwa: 18/12/2021