33. Maiti aswaliwe na imamu wa msikiti au aliyeachiwa wasia?

Swali 33: Maiti akiwa ameacha anausia aswaliwe na mtu maalum. Je, mtu huyu ana haki zaidi kuliko imamu mteulie[1]?

Jibu: Imamu wa msikiti ana haki zaidi ya kuswalia jeneza kuliko mtu aliyeacha anausiwa. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Mtu asimwongoze mwengine kabisa katika utawala wake.”[2]

Imamu wa msikiti ndiye mwenye utawala msikitini mwake.

[1] Majmuu´-ul-Fataawaa (13/137).

[2] Muslim (673).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahkaam-ul-Janaa-iz, uk. 28-29
  • Imechapishwa: 19/12/2021