Daku inayo baraka za kidini na za kidunia. Isitoshe ni kutekeleza amri ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na kumfuata. Ikiwa mwenye kula daku ataweka nia ya kufuata amri ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na kumfuata, basi kula kwake daku kunakuwa ni ´ibaadah yenye thawabu. Katika kula daku kuna kujitofautisha na watu wa Kitabu ambao ni mayahudi na manaswara. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Kipambanuzi kati ya funga yetu na funga ya watu wa Kitabu ni kula daku.”[1]
Miongoni mwa baraka za daku husaidia mwili kuwa na nguvu kwa ajili ya ´ibaadah na kuchunga nguvu za mwili na uchangamfu wake. Mwenye kula daku anakuwa na nguvu zaidi katika kutekeleza majukumu yake ya kila siku kuliko yule asiyekula dakula.
Miongoni mwa baraka za daku husaidia mtu kuamka mwisho wa usiku kwa ajili ya kufanya Dhikr, du´aa na swalah, ambayo ni wakati wenye matarajio makubwa ya kujibiwa maombi.
Kwa hivyo mtu anatakiwa kupupia kula daku na kusimpite hata kama hana hamu. Kwani daku inafikiwa kwa kutumia kile kiasi kidogo mno cha chakula au kunywa kitu – hata ikiwa ni funda moja ya maziwa – ili apate baraka hizi na faida hizi kubwa – na Allaah ndiye mwenye kutakwa msaada.
[1] Muslim (1096).
- Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Minhat-ul-´Allaam fiy Sharh Buluugh-il-Maraam (05/30)
- Imechapishwa: 09/02/2025
Daku inayo baraka za kidini na za kidunia. Isitoshe ni kutekeleza amri ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na kumfuata. Ikiwa mwenye kula daku ataweka nia ya kufuata amri ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na kumfuata, basi kula kwake daku kunakuwa ni ´ibaadah yenye thawabu. Katika kula daku kuna kujitofautisha na watu wa Kitabu ambao ni mayahudi na manaswara. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Kipambanuzi kati ya funga yetu na funga ya watu wa Kitabu ni kula daku.”[1]
Miongoni mwa baraka za daku husaidia mwili kuwa na nguvu kwa ajili ya ´ibaadah na kuchunga nguvu za mwili na uchangamfu wake. Mwenye kula daku anakuwa na nguvu zaidi katika kutekeleza majukumu yake ya kila siku kuliko yule asiyekula dakula.
Miongoni mwa baraka za daku husaidia mtu kuamka mwisho wa usiku kwa ajili ya kufanya Dhikr, du´aa na swalah, ambayo ni wakati wenye matarajio makubwa ya kujibiwa maombi.
Kwa hivyo mtu anatakiwa kupupia kula daku na kusimpite hata kama hana hamu. Kwani daku inafikiwa kwa kutumia kile kiasi kidogo mno cha chakula au kunywa kitu – hata ikiwa ni funda moja ya maziwa – ili apate baraka hizi na faida hizi kubwa – na Allaah ndiye mwenye kutakwa msaada.
[1] Muslim (1096).
Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Minhat-ul-´Allaam fiy Sharh Buluugh-il-Maraam (05/30)
Imechapishwa: 09/02/2025
https://firqatunnajia.com/21-daku-baraka-zake-za-kidini-na-kilimwengu/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)