95 – Muhammad amesema: Qaadim ad-Daylamiy amenihadithia: Nimemsikia Abu Safwaan al-´Aabid akisema:

”Ilikuwa inasema kuwa njaa inawafanya wale wenye kuhisi njaa kuona kwa nuru ya Allaah wakati wanapotazama utukufu Wake kwa viumbe Wake. Na ilikuwa inasemwa kwamba msingi wa utukufu unapatikana katika kujitosheleza, utegemezi unatosha, uchaji ni raha na ´ibaadah inapelekea katika utulivu. Mtu hajakosa kitu chenye madhara madogo zaidi kwake kama chakula alichokiacha kwa ajili ya Allaah. Bali ni jambo linapelekea mwisho mwema kwa wale wenye kumcha Allaah.”

96 – al-Husayn bin ´Abdir-Rahmaan ametuhadithia, kutoka kwa bwana mmoja katika Banu Tamiym, aliyesema:

”al-A´mash alimwambia bwana mmoja: ”Ee mpumbavu, unaona tumbo hili? Ukilitweza, litakuheshimisha, na ukiliheshimisha, litakutweza.”

97 – al-Husayn bin ´Abdir-Rahmaan amenihadithia: al-Hasan, au mtu mwingine, amesema:

”Janga la baba yenu Aadam ilikuwa katika kula. Nanyi mtakuwa na janga hilohilo mpaka siku ya Qiyaamah.”

98 – al-Husayn bin ´Abdir-Rahmaan amenihadithia: Maalik bin Diynaar amesema:

”Kushiba kunaufanya moyo kuwa mgumu na kuubwetesha mwili.”

99 – al-Husayn bin ´Abdir-Rahmaan amenihadithia: Maalik bin Diynaar amesema:

”Yule mwenye kulimiliki tumbo lake, basi atamiliki matendo mema yote.”

100 – al-Husayn bin ´Abdir-Rahmaan amenihadithia:

”Ilikuwa inasemwa kwamba kula sana kunaufisha moyo kama jinsi maji mengi yanafisha mazao.”

101 – al-Husayn amenihadithia: ´Abdur-Rahmaan bin Zayd amesema:

”Kitu cha kwanza ambacho muumini anakifanyia kazi ni tumbo lake; tumbo lake likikaa katika msitari basi dini yake hukaa katika msitari, na tumbo lake lisipokaa katika msitari basi dini yake haikai katika msitari.”

102 – al-Husayn bin ´Abdir-Rahmaan amenihadithia akasema:

”Ilikuwa inasemwa: ”Hekima haiishi katika tumbo lililojaa.”

  • Mhusika: Imaam Abu Bakr ´Abdullaah bin Muhammad bin Abiyd-Dunyaa
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-ul-Juu´, uk. 77-78
  • Imechapishwa: 23/07/2023