22. Usilifanye tumbo lako ikawa ndio hamu yako kubwa

103 – Muhammad bin Idriys amenihadithia: Ahmad bin Abiyl-Hawaariy amesema: Nimemsikia Abu Sulaymaan ´Abdur-Rahmaan bin Ahmad bin ´Atwiyyah al-´Ansiy ad-Daariy akisema kuhusu maneno Yake (´Azza wa Jall):

وَجَزَاهُم بِمَا صَبَرُوا جَنَّةً وَحَرِيرًا

”Atawalipa kwa sababu ya kusubiri kwao, Pepo na nguo za hariri.”[1]

”Bi maana subira yao kutokana na matamanio.”

104 – Haaruun bin ´Abdillaah ametuhadithia: Sayyaar ametuhadithia: Ja´far ametuhadithia:

”Tulikuwa kwa Maalik bin Diynaar, akaja Hishaam bin Hassaan akasema: ”Yuko wapi Abu Yahyaa?” Tukasema: ”Kwa muuza mboga.” Akasema: ”Tumwendee.” Nikamtazama Hishaam ambapo akasema: ”Ee Hishaam! Mimi kila mwezi humpa muuza mboga huyu dirhamu 1.20 na nikachukua kutoka kwake mikate sitini; mikate miwili kila jioni. Nikiipasha moto, sihitaji cha kuweka juu yake. Mimi nimesoma katika Zabuur ya Daawuud (´alayhis-Salaam): ”Mungu Wangu, hakika umeona masononeko yangu kutokea juu.” Tazama masononeko yako, ee Hishaam.”

105 – Muhammad bin al-Husayn ametuhadithia: ´Ubaydullaah bin Muhammad at-Taymiy ametuhadithia: Muhammad bin Mis´ar ametuhadithia: Maalik amesema:

”Haitakikani kwa muumini tumbo ndio iwe hamu yake kubwa. Wala haitakiwi matamanio yake yawe ndio yenye kummiliki.”

106 – Amesema vilevile:

”Maalik bin Diynaar alikutana na kijakazi ambaye alikuwa jirani yake, kisha baadaye akauzwa. Akamuuliza: ”Je, ni mwanamke fulani?” Akasema: ”Ndio, ee Abu Yahyaa.” Akasema: ”Unaendelejae? Ni vipi mahali pako papya?” Mwanamke yule akasema: ”Nimtoe fidia baba yangu kwako! Hali yao ni nzuri kiasi gani! Nyumba zao zimestawi kiasi gani!” Akasema: ”Je, wanawatendea watu wema?” Mwanamke yule akasema: ”Ee Abu Yahyaa! Nyumba zao zimestawi na chakula chao ni kingi!” Ndipo Abu Yahyaa akasema: ”Mimi namuuliza juu ya wema wao kwa watu na yeye ananieleza anayeenda msalani.”

107 – Muhammad amesema: Muhammad bin Yaziyd bin Khunays ametuhadithia: ´Abdul-´Aziyz bin Abiy Rawaad amesema:

”Ilikuwa inasemwa kwamba chakula kichache kinachangia kuharakia kufanya matendo mema.”

[1] 76:12

  • Mhusika: Imaam Abu Bakr ´Abdullaah bin Muhammad bin Abiyd-Dunyaa
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-ul-Juu´, uk. 79-81
  • Imechapishwa: 19/07/2023