Waislamu na siku ya ´Aashuuraa´

Swali: Unaweza kukumbusha kuhusu kufunga siku ya ´Aashuuraa´? Ni ipi hukumu ya wale wanaojipiga makofi?

Jibu: Sifa zote njema ni stahiki ya Allaah juu ya kwamba waislamu hawajipigi makofi, hawaombolezi wala kuonyesha hasira. Mambo yalivyo ni kwamba wanatendea kazi Sunnah. Wanafunga siku ya ´Aashuuraa´ na siku moja kabla yake au siku moja baada yake kwa ajili ya kujitofautisha na mayahudi. Ni Sunnah iliyokokotezwa. Ni Sunnah iliyokokotezwa kufunga ´Aashuuraa´.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.alfawzan.af.org.sa/node/14251
  • Imechapishwa: 19/07/2023