Kalenda ili kuweza kuilenga siku ya ´Aashuuraa´?

Swali: Mimi ni kijana ambaye Allaah ameniongoza katika haki na nataka kufunga ´Aashuuraa´ na masiku mengine yote yenye ubora yasiyokuwa Ramadhaan. Je, tutegemee kalenda wakati wa kufunga ´Aashuuraa´ ili kuweza kulenga ile siku umeanza mwezi wa Allaah Muharram? Au salama zaidi ni mtu afunge siku moja kala na baada yake?

Jibu: Ni lazima kwako kutegemea mwezi mwandamo. Usipoona mwezi mwandamo basi chukua tahadhari; nako ni kule kukamilisha Dhul-Hijjah siku thelathini.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (15/402)
  • Imechapishwa: 19/07/2023