89 – Muhammad bin Qudaamah al-Jawhariy amenihadithia: Marwaan bin Mu´aawiyah ametuhadithia, kutoka kwa Abu Daawuud ar-Ruumiy, ambaye amesema:

”Bwana mmoja alimwambia ´Umar bin ´Abdil-´Aziyz: ”Je, tusikutengenezee dawa itayofanya kutamani chakula?” Akasema: ”Niifanye nini?” Naapa kwa Allaah! Mimi huingia msalani na nikaudhiwa na kile chenye kunitoka.” Wakasema: ”Je, tusikutengenezee dawa itayofanya kutamani wanawake?” Akasema: ”Niifanye nini? Naapa kwa Allaah! Wakati fulani hujiwa na jambo hilo, ambapo nikapatwa na kughafilika na uchangamfu.”

90 – Humayd bin Ahmad ameeleza kutoka kwa Sufyaan bin ´Uyaynah, ambaye amesimulia kwamba ´Aliy [tupu]:

”Wakati mwingine mtu hula kushiba ambapo mwili wake ukachupa mipaka.”

91 – Muhammad bin Qudaamah amenihadithia: Nimemsikia Muusa bin Daawuud akisema: Nimemsikia Maalik bin Anas akisema:

”Tumefikiwa na khabari kwamba kulisemwa kuambiwa Ibn ´Umar: : ”Tusikupikie uji wa ngano?” Akasema: ”Na ni kitu gani huo uji wa ngano?” Akasema: ”Ni kitu ambacho hulainisha hisia zako za shibe unapokuwa umekula na ukashiba.”Ni kitu ambacho ikiwa umekula kushiba, kinakufaa.” Ndipo akasema: ”Sijashiba tangu alipouliwa ´Uthmaan.”

92 – Muhammad bin ´Abdil-Majiyd at-Tamiymiy amenihadithia: Nimemsikia Yuusuf bin al-Asbaatw akisema:

”Njaa inaulainisha moyo.”

93 – Muhammad bin al-Husayn ametuhadithia: Bishr bin Muslih amenihadithia: Nimemsikia Yuusuf bin al-Asbaatw akisema:

”Njaa ndio msingi wa kila mtu mwema ardhini.”

 94 – Muhammad amesema: Ahmad bin Sahl al-Urduniy amenihadithia: Abu Farwah al-Answaariy ametuhadithia, kutoka kwa as-Sarriy bin Yan´um, ambaye amesema:

”Ilikuwa inasemwa kwamba mja hatohisi njaa isipokuwa Allaah badala yake ataweka mahali pake hekima na uchaji. Ilikuwa pia inasemwa kwamba njaa ni nembo ya Mitume na waja wema.”

  • Mhusika: Imaam Abu Bakr ´Abdullaah bin Muhammad bin Abiyd-Dunyaa
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-ul-Juu´, uk. 74-77
  • Imechapishwa: 20/06/2023