72 – Daawuud bin ´Amr adh-Dhwabbiy ametuhadithia: Ya´quub bin Muhammad bin Twahlaa’ ametuhadithia, kutoka kwa ´Ubayd bin Sulaymaan, kutoka kwa Ya´quub bin ´Abdillaah al-Ashajj, aliyesimulia kuwa alifikiwa na khabari kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alisema:

”Tamaa ni mbaya.”

73 – ´Aliy bin al-Ja´d ametuhadithia: al-Mubaarak bin Fadhwalah amenikhabarisha, kutoka kwa al-Hasan, ambaye amesema:

”Kulisemwa kuambiwa Samurah bin Jundub: ”Mwanao alikula kwa ulafi usiku wa jana.” Akasema: ”Angelikufa, basi nisingelimswalia.”

74 – Suraydj bin Yuunus amenihadithia: Hushaym ametukhabarisha, kutoka kwa Mansuur, kutoka kwa al-Hasan, ambaye amesema:

”Luqmaan alisema kumwambia mwanae: ”Usile wakati umeshiba. Mtupie mbwa chakula kilichobaki.”

75 – Haashim bin al-Haarith ametuhadithia: ´Ubaydullaah bin ´Amr ar-Raqqiy ametuhadithia, kutoka kwa ´Abdullaah bin Muhammad bin ´Uqayl, kutoka kwa Jaabir, ambaye amesema:

”Niliswali ´Aswr pamoja na Abu Bakr, kisha nikaandamana naye nyumbani kwake. Akamwambia mke wake Asmaa’ bint ´Umays: ”Je, unacho chakula?” Akasema: ”Hapana, naapa kwa Allaah, hakuna chochote.” Akasema: ”Tazama.” Akasema: ”Hapana, naapa kwa Allaah, hakuna chochote.” Akamchukua kondoo jike ambaye alikuwa amezaa siku hiyohiyo na akamkamua maziwa yake. Akayamimina ndani ya chungu na akamuamuru kijakazi wake kuyapika. Baadaye tukaletewa. Tukala ambapo tukaomba pasi na kutawadha.”

76 – Surayj bin Yuunus ametuhadithia: Hushaym ametuhadithia , kutoka kwa Ismaa´iyl bin Abiy Khaalid, ambaye ameeleza:

”Bwana mmoja alikuja kwa Ibn ´Umar akasema: ”Tusikupikie uji wa ngano?” Akasema: ”Na ni kitu gani huo uji wa ngano?” Akasema: ”Ni kitu ambacho hulainisha hisia zako za shibe unapokuwa umekula na ukashiba.” Ndipo Ibn ´Umar akasema: ”Sijashiba tangu miezi minne iliyopita. Na si kwamba eti sikipati, lakini nina uzoefu wa watu ambao wakati fulani wanahisi njaa na wakati mwingine wanashiba.”

  • Mhusika: Imaam Abu Bakr ´Abdullaah bin Muhammad bin Abiyd-Dunyaa
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-ul-Juu´, uk. 67-70
  • Imechapishwa: 20/06/2023