Matakwa ya Allaah na Mtume katika mambo ya dunia

Mambo ya Shari´ah inajuzu kusema “Allaah na Mtume Wake ndio wanajua zaidi”. Lakini kuhusu na mambo ya kilimwengu hutakiwi kusema “Allaah na Mtume Wake…” Badala yake sema “Allaah kisha Mtume…” Wakati mtu alipomwambia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Akitaka Allaah na wewe.”

Akasema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Umenifanya kuwa mshirika wa Allaah. Badala yake sema “Akitaka Allaah peke yake.”[1]

[1]Ahmad (01/214).

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Riyaadh-is-Swaalihiyn (01/483)
  • Imechapishwa: 20/06/2023