Mtu kuuliza maswali anayoyajua ili kuwanufaisha wengine

Katika Hadiyth hii – Hadiyth ya Jibriyl – kuna dalili mtu akiuliza kuhusu kitu anachokijua kwa ajili ya kuwanufaisha wengine, basi mtu huyu anakuwa ni mwenye kuwafunza. Kwa sababu aliyejibu ni Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Jibriyl ndio aliyeuliza na sio yeye aliyewafunza watu. Lakini yeye ndiye alikuwa sababu ya jibu hili ambalo watu walinufaika nalo.

Wanachuoni wamesema inatakiwa kwa mwanafunzi pindi anapokaa na mwanachuoni katika kikao, aulize juu ya mambo muhimu kwa waliohudhuria pale hata kama yeye atakuwa anajua hukumu yake. Lengo ni ili awanufaishe walioko pale na awe ni mwenye kuwafunza.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Riyaadh-is-Swaalihiyn (01/482-483)
  • Imechapishwa: 20/06/2023