Mtu akikuuliza ni zipi hizo tanzu sabini na tatu, atajibiwa kwamba hatukutajiwa zote kwa pamoja mpaka tuweze kuzitaja. Hata kama inatambulika kwamba hazikutajwa zote kwa pamoja katika Hadiyth moja, lakini kwa hali yoyote ni katika kumtii na kumcha Allaah. Ukiyazingatia mapokezi mbalimbali, utazipata hapa na pale. Hujui kwamba kuondosha madhara kutoka katika njia ni sehemu katika imani? Vivyo hivyo maneno yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Hayaa ni tanzu katika imani.”[1]

“Ghera ni katika imani.”[2]

“Uchakavu ni katika imani.”[3]

“Agano jema ni katika imani.”[4]

Yote haya ni katika matawi ya imani. ´Ammaar (Radhiya Allaahu ´anh) amepokea yafuatayo:

“Mambo matatu ni katika imani; kujitolea wakati wa hali ngumu, kuifanyia uadilifu nafsi yako na kuwatolea salamu walimwengu.”[5]

[1] al-Bukhaariy na Muslim. Tazama ”al-Iymaan” (66) ya Ibn Abiy Shaybah.

[2] al-Bazzaar na Ibn Battwah katika ”al-Ibaanah” kupitia kwa Abu Sa´iyd, kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), kwa cheni ya wapokezi ambayo iko na mpokezi ambaye hali yake haijulikani.

[3] Abu Daawuud, Ibn Maajah na wengineo kupitia kwa Abu Umaamah al-Haarithiy, kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). al-Haakim ameisahihisha na adh-Dhahabiy akaafikiana naye.

[4] Nzuri. Swahiyh kwa mujibu wa al-Haakim. Imetajwa katika ”Silsilat-ul-Ahaadiyth as-Swahiyhah”.

[5] Imepokelewa kama maneno ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na pia kama maneno ya ´Amaamar. Maoni yenye nguvu ni kwamba ni maneno ya ´Ammaar ingawa katika cheni ya wapokezi kuna mkanganyiko.

  • Mhusika: Imaam Abu ´Ubayd al-Qaasim bin Sallaam
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-ul-Iymaan, uk. 27-29
  • Imechapishwa: 21/06/2023
  • taaliki: Imaam Muhammad Naawswir-ud-Diyn al-Albaaniy