19. Mtu mnene wakati wa Salaf

82 – Muhammad amesema: Abu ´Umar adh-Dhwariyr ametuhadithia: al-Hasan bin Diynaar ametuhadithia, kutoka kwa al-Hasan, ambaye amesema:

”Hapo kitambo ilikuwa ni aibu kwa muislamu kuambiwa kuwa wewe ni mnene.”

83 – Muhammad amesema: ´Ubaydullaah bin Muhammad at-Taymiy ametuhadithia: Salamah bin Sa´iyd ametuhadithia:

”Mtu alikuwa anaweza kusemwa vibaya kwa unene kama anavosemwa vibaya kwa dhambi aliyofanya.”

84 – Nimehadithiwa kutoka kwa al-Mu´aafaa bin ´Imraan, kutoka kwa Sufyaan ath-Thawriy, kutoka kwa ´Amr bin Qays al-Malaa-iy, ambaye amesema:

”Jihadharini na unene. Hakika unaufanya moyo kuwa mgumu.”

85 – al-Husayn bin ´Abdir-Rahmaan amenihadithia: Baadhi ya wanazuoni wamesema:

”Ikiwa wewe ni mnene, basi jizingatie kuwa mgonjwa mpaka pale utakapopungua.”

86 – Ameeleza tena kuwa Ibn-ul-A´raabiy amesema:

”Waarabu walikuwa wakiona kuwa mtu halali akiwa ni mnene akawa ni mwenye maamuzi.”

87 – Abu Haatim ar-Raaziy amenihadithia, kutoka kwa Ahmad bin Abiyl-Hawaariy: Abu Sulaymaan amesema:

”Unapotaka kufanya jambo miongoni mwa mambo ya kidunia na Aakhirah, basi usile mpaka umelifanya. Kwani hakika kula kunaibadilisha akili.”

88 – ´Aliy bin Ja´far al-Ahmar amesema: Nimemsikia baba yangu akisema kuwa Ayyuub alikuwa akisema:

”Kula sana ni maradhi ya tumbo na ni kuzidi kuoza.”

  • Mhusika: Imaam Abu Bakr ´Abdullaah bin Muhammad bin Abiyd-Dunyaa
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-ul-Juu´, uk. 72-74
  • Imechapishwa: 20/06/2023