19. Malipo kwa ajili ya kuswalisha Tarawiyh

Swali: Ni ipi hukumu ya kumpangia imamu kikomo cha malipo yake kwa kuwaswalisha kwake watu khaswa ikiwa anaenda maeneo ya mbali kuwaswalisha watu Tarawiyh?

Jibu: Haitakikani kumpangia kikomo. Ni jambo wamelichukia wengi katika Salaf. Ni sawa endapo watamsaidia kwa kitu kisichokuwa na kikomo. Kuhusu swalah ni sahihi na haina neno – Allaah akitaka – hata kama watampangia kikomo cha msaada. Kwa sababu haja inaweza kupelekea katika jambo hilo. Lakini anatakiwa asifanye hivo na msaada uwe pasi na kuwekewa masharti. Hivi ndivo bora na salama zaidi, kama walivosema kikosi cha Salaf (Rahimahumu Allaah). Anaweza kufarijika kwa maneno yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kumwambia ´Uthmaan bin Abiyl-´Aasw (Radhiya Allaahu ´anhumaa):

“Chukua muadhini na asipokee malipo kwa ajili ya adhaana yake.”[1]

Ikiwa hali ndio hii kwa muadhini basi imamu ana haki zaidi.

Kinacholengwa si sawa kuweka sharti kwa ajili ya kuwaswalisha watu. Watu wakimsaidia kwa kile kinachomsaidia kulipa gari, basi jambo hilo ni zuri pasi na kuwawekea sharti.

[1] Wameipokea watano na ni nzuri kwa mujibu wa at-Tirmidhiy. Ameisahihisha al-Haakim. Ameyataja hayo al-Haafidh [Ibn Hajar] katika ”al-Buluugh”.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Swalaat-it-Taraawiyh, uk. 20
  • Imechapishwa: 15/04/2022