20. Tahajjud na Tarawiyh inakuwa baada ya Raatibah ya ´Ishaa

Swali: Baada ya kumaliza swalah ya ´Ishaa kuna waswaliji ambao huswali Sunnah kabla ya kuanza swalah ya Tarawiyh. Ni kwa nini baada ya kufanya Istighfaar, Tahliyl, Tasbiyh imamu asiingie moja kwa moja katika swalah ya Tarawiyh pasi na kuswali Rak´ah hizi mbili za Sunnah?

Jibu: Sunnah ni Tahajjud, katika Ramadhaan na miezi mingine, iwe baada ya Sunnah ya Raatibah ya ´Ishaa. Hivo ndivo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alivokuwa akifanya. Hapana tofauti katika hayo kati ya Tahajjud iwe msikitini au nyumbani.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Swalaat-it-Taraawiyh, uk. 21
  • Imechapishwa: 15/04/2022