17 – ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa) ameeleza:

“Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akibusu hali ya kuwa amefunga na akichanganyikana ilihali amefunga, lakini alikuwa ni mwenye kuweza kujizuia vyema kuliko nyinyi.”

Ameipokea al-Bukhaariy na Muslim. Imekuja katika upokezi wa Muslim:

“Alikuwa akibusu katika mwezi wa funga.”[1]

Hadiyth hii ni dalili juu ya kwamba inafaa kwa mfungaji kumbusu na kutangamana na mke wake. Hapana tofauti katika hali kati ya swawm ya faradhi na swawm iliyopendekezwa muda wa kuwa hachelei kuamsha matamanio yake na kutokwa na kitu katika manii kwa sababu ni yenye kutoka kwa haraka au anachelea jambo hilo kumvutia katika jimaa. Katika hali hiyo itamlazimu kuacha kubusu na kutangamana kwa minajili ya kuzuia njia. Jengine ni kwa sababu ni lazima kuichunga swawm kutokamana na mambo yanayoiharibu. Kitu ambacho hakitimii kitu cha wajibu isipokuwa kwacho basi kitu hicho pia kitakuwa ni wajibu. Isitoshe Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amemwamrisha mwenye kutawadha kufanya kishindo wakati wa kupandisha maji puani. Isipokuwa akiwa amefunga ili maji yasiingie tumboni mwake. Vivyo hivyo kutazuiliwa kubusu ikiwa kunapelekea katika jimaa inayoharibu swawm. Imefahamisha jambo hilo maneno yake (Radhiya Allaahu ´anhaa):

“… lakini alikuwa ni mwenye kuweza kujizuia vyema kuliko nyinyi.”

Maana yake ni kwamba mnatakiwa kujihadhari kutokamana na kubusu na wala msifikiri kuwa nyinyi ni kama Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) katika kuhalalishwa kwake. Yeye anaweza kuimiliki nafsi yake na anajiaminisha kutokea chochote. Ndani yake kuna ishara kuwa ambaye hamiliki matamanio yake basi jambo hilo litamdhuru[2].

Makusudio ya kuchanganyikana (المباشرة) ni kukutana ngozi mbili na ni jambo limeenea zaidi kuliko kubusu. Wakati mwingine inatumiwa juu ya jimaa. Lakini sio kilichokusudiwa hapa. Ametaja kuchanganyikana baada ya kubusu kwa njia ya kutaja kilichoenea baada ya kilicho maalum. Kwa sababu kubusu ni kitu maalum kuliko kuchanganyikana.

Mfungaji akibusu au akachanganyikana na hivyo akatokwa na manii, basi swawm yake inaharibika. Atalazimika kulipa kwa mujibu wa maoni ya kikosi cha wanazuoni wengi. Kafara ni kitu maalum juu ya jimaa. Lakini analazimika kutubu, kujutia, kuomba msamaha na kujiepusha na mambo haya yanayoamsha matamanio. Kwani yuko ndani ya ´ibaadah tukufu. Allaah (Ta´ala) amesema juu yake:

”Anaacha chakula kwa ajili Yangu, anaacha kinywaji kwa ajili Yangu, anaacha ladha yake kwa ajili Yangu na anamwacha mke wake kwa ajili Yangu.”[3]

Kwa hivyo mfungaji anatakiwa kuacha ladha na matamanio yake yote. Katika jumla ya hayo kunaingia kutokwa na manii[4].

Akitokwa na madhiy kwa ajili ya kuchanganyikana au kubusu swawm yake haitoharibika kwa mujibu wa maoni sahihi zaidi ya wanazuoni. Kilichotoka hicho hakilazimishi mtu kuoga. Kimefanana na mkojo.

Mfungaji anatakiwa kupupia kujiepusha na kila kinachomtumbukia katika madhara na kutia kasoro swawm yake au kupunguza thawabu zake. Hakika kufanya hivo ni katika kuadhimisha maamrisho na makatazo ya Allaah. Amesema (Ta´ala):

ذَٰلِكَ وَمَن يُعَظِّمْ حُرُمَاتِ اللَّـهِ فَهُوَ خَيْرٌ لَّهُ عِندَ رَبِّهِ

“Ndio hivyo iwe na yeyote anayetukuza vitukufu vya Allaah, basi hivyo ni kheri kwake mbele ya Mola wake.”[5]

Allaah ndiye mjuzi zaidi.

Ee Allaah! Tufishe hali ya kuwa ni waumini na tuunganishe na waja wema. Ee Allaah! Tuwafikishe tawfiyq yenye yakini kuepuka kukuasi, tuelekeze kuyakimbilia yanayokuridhisha, tupe mema ya dunia hii na mema ya Aakhirah na tukinge na adhabu ya Moto.

[1] al-Bukhaariy (1927) na Muslim (1106).

[2] al-Mu´allim bifawaaid Muslim (02/33-34).

[3] Swahiyh Ibn Khuzaymah (03/197). Tazama ”Fath-ul-Baariy” (04/107).

[4] Tarjiyh fiy Masaail-is-Swawm waz-Zakaah, uk. 96 kwa hati ya mkono ya Muhammad bin ´Umar Bazmuul.

[5] 22:30

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Mukhtaswar Ahaadiyth-is-Swiyaam, uk. 49-50
  • Imechapishwa: 28/04/2022