Na Kasema alivyosema (Ta´ala):

لَهُ دَعْوَةُ الْحَقِّ ۖ وَالَّذِينَ يَدْعُونَ مِن دُونِهِ لَا يَسْتَجِيبُونَ لَهُم بِشَيْءٍ

“Kwake ndiko kuna maombi yote ya haki. Na wale wanaoomba pasi Naye hawawaitikii kwa chochote.” (ar-Ra´d 13 : 14)

MAELEZO

Kwake ndiko kuna maombi… – Bi maana ´ibaadah sahihi. Amesema (Ta´ala):

أَلَا لِلَّـهِ الدِّينُ الْخَالِصُ

“Tanabahi! Ni ya Allaah pekee dini iliyotakasika.” (39:03)

Allaah (Jalla wa ´Alaa) hakubali isipokuwa tu maombi ya haki ambayo ni ile dini takasifu. Kuhusiana na ambaye anamuabudu Allaah na wakati huo huo anaabudu wengine pamoja Naye, haya ni maombi ya shirki yasiyokubaliwa na Allaah. Amesema:

وَالَّذِينَ يَدْعُونَ مِن دُونِهِ

“Na wale wanaoomba pasi Naye… “

Ni yenye kuenea kwa kila kile chenye kuombwa badala Yake. Haijalishi kitu ikiwa ni Malaika, Mtume, mja mwema, sanamu au kitu kingine chochote kile. Amesema:

لَا يَسْتَجِيبُونَ لَهُم بِشَيْءٍ

“… hawawaitikii kwa chochote.”

Hawawezi kuwajibu kwa kitu kwa kuwa si waweza. Hawana uwezo wa kitu.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Kashf-ish-Shubuhaat, uk. 28
  • Imechapishwa: 15/10/2016