16. Mtume aliwapiga vita washirikina kwa ajili ya shirki zao

na ukajua ya kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kawapiga vita kwa ajili ya shirki hii na akawaita kumtakasia ´Ibaadah Allaah pekee. Kama Alivyosema (Ta´ala):

وَأَنَّ الْمَسَاجِدَ لِلَّـهِ فَلَا تَدْعُوا مَعَ اللَّـهِ أَحَدًا

“Na kwamba mahala pote pa kuswalia ni kwa ya Allaah, hivyo basi msiombe yeyote pamoja na Allaah.” (al-Jinn 72 : 18)

MAELEZO

Ukitambua ya kuwa ´ibaadah zao pamoja na shirki hazikuwafaa kitu kwa kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hakuwakubalia. Bali aliwalingania kumpwekesha Allaah kwa ´ibaadah na kuacha kuabudu asiyekuwa Yeye. Aayah hii inakataza kuwaabudu Malaika, Mitume na waja wema. Ndani yake kuna kubatilisha kuabudiwa asiyekuwa Yeye (´Azza wa Jall) – yoyote awaye – hata kama watu wake hawaamini kuwa wanaumba au wanaruzuku bali tu wanawaonelea kuwa ni waja wema wanaowafanya kuwa wakati kati na kwamba ni waombezi wao wanaowakurubisha mbele ya Allaah (´Azza wa Jall). Amesema (Ta´ala):

وَيَعْبُدُونَ مِن دُونِ اللَّـهِ مَا لَا يَضُرُّهُمْ وَلَا يَنفَعُهُمْ وَيَقُولُونَ هَـٰؤُلَاءِ شُفَعَاؤُنَا عِندَ اللَّـهِ

“Wanaabudu badala ya Allaah visivyowadhuru wala kuwanufaisha na wanasema: “Hawa ni waombezi wetu mbele ya Allaah.”” (10:18)

Hii leo wanasema kuwa ni waombezi wao ambao wanatawasali kwao kumfikia Allaah (´Azza wa Jall). Haya yote ndio dini ya kipindi cha kishirikina ambayo ni batili. Kwa kuwa inahusiana na kumuabudu asiyekuwa Allaah (´Azza wa Jall).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Kashf-ish-Shubuhaat, uk. 27
  • Imechapishwa: 15/10/2016