15. Tunamhukumu mtu kutegemea na yale yanayodhihiri kwake

Kuna wanaosema haifai kumhukumu mtu ukafiri wala ushirikina – pasi na kujali chochote kile atakachofanya au atakachosema – mpaka yajulikane yale yaliyomo ndani ya moyo wake. Ametakasika Allaah! Sisi tunajua yale yaliyomo kwenye mioyo au ni Allaah ndiye anayejua yaliyomo ndani ya moyo? Sisi tunahukumu yale tunayoyaona kwa nje. Kuhusu yaliyoko ndani hakuna ayajuaye isipokuwa Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) pekee. Mwenye kufanya shirki anahukumiwa kuwa ni mshirikina na atatangamiwa kama mshirikina mpaka pale atapotubu kwa Allaah (Ta´ala) na kushikamana na ´Aqiydah ya Tawhiyd. Kadhalika yule mwenye kuitendea kazi Tawhiyd na kutamka shahaadah atatangamiwa kama muislamu midhali hakujadhihiri kutoka kwake yale yanayotengua hilo. Tunatangamana na kila mmoja kutegemea na yale yanayodhihiri kutoka kwake.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Kashf-ish-Shubuhaat, uk. 26
  • Imechapishwa: 15/10/2016