14. Washirikina walikuwa wakitofautiana katika ´ibaadah zao

Halafu katika wao kulikuwa wanaowaomba Malaika kwa ajili ya wema wao na ukaribu wao kwa Allaah ili wawaombee, au wanamuomba mtu mwema, kama mfano wa Laat, au Mtume kama mfano wa ´Iysa – na ukajua ya kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kawapiga vita kwa ajili ya shirki hii na akawaita kumtakasia ´Ibaadah Allaah pekee. Kama Alivyosema (Ta´ala):

وَأَنَّ الْمَسَاجِدَ لِلَّـهِ فَلَا تَدْعُوا مَعَ اللَّـهِ أَحَدًا

“Na kwamba mahala pote pa kuswalia ni kwa ya Allaah, hivyo basi msiombe yeyote pamoja na Allaah.” (al-Jinn 72 : 18)

MAELEZO

Washirikina hawa walikuwa ni wenye kutofautiana katika ´ibaadah zao. Miongoni mwao kuna waliokuwa wakiwaabudu Malaika, wengine wakimuabudu ´Iysaa, mwana wa Maryam, wengine wakiwaabudu waja wema. Hii ndio ilikuwa dini ya washirikina. Jambo la kusikitisha ndio uhalisia wa mambo katika sehemu kubwa ya ulimwengu wa Kiislamu hii leo. Wanamuabudu Allaah kwa kuhiji, kufunga na kuswali lakini hata hivyo wanatumbukia katika shirki kubwa. Utawaona ni wenye kuwaabudu maiti, wanawachinjia na wanawataka msaada. Unaweza kupata watu wasioijua Tawhiyd wanaowapa udhuru watu kama hawa na kusema kuwa ni wenye udhuru kwa kuwa hawaitakidi kuwa maiti hawa wanaumba na kwamba wanaruzuku na kwamba wanawafanya wakati kati tu na waombezi. Akisikia haya sana utamsikia anasema kuwa watu hawa ni wenye kukosea. Si ajabu vilevile akasema kuwa watu hawa ni wenye kufanya Ijtihaad na hivyo wana ujira mmoja. Huenda vilevile akasema kuwa watu hawa ni wajinga. Vipi watakuwa wajinga ilihali Qur-aan inasomwa kwao na Hadiyth zinasikiwa na maneno ya wanachuoni wanarudiliwarudiliwa? Uhakika wa mambo ni kwamba hawa ni wakaidi. Wameshasimamishiwa dalili lakini hata hivyo hawakubali.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Kashf-ish-Shubuhaat, uk. 26
  • Imechapishwa: 15/10/2016