13. Waislamu wa leo wanaokumbushia washirikina wa ki-Quraysh

Wale ambao wanadai Uislamu hii leo na wanaswali, wanafunga na wanahiji lakini wakawa wanamuomba al-Husayn, al-Badawiy na ´Abdul-Qaadir al-Jaylaaniy. Hawa ni kama wale washirikina wa mwanzo. Washirikina hawa walikuwa wakimuabudu Allaah (´Azza wa Jall) lakini wakimuomba al-Laat, al-´Uzzaa, Manaat mwengine wa tatu. Hawasemi kuwa hawa ni waungu wao. Wanachosema ni kuwa hawa wanawakurubisha mbele ya Allaah na kwamba wanataka kutoka kwao wawakurubishe kwa Allaah na kwamba eti ni waombezi wao baina yao na Allaah. Hawa pia wanasema kuwa al-Hasan, al-Husayn, al-Hasan, ´Abdul-Qaadir na al-Badawiy ni waombezi wao mbele ya Allaah na hawasemi kuwa wanaumba, wanaruzuku au wanaendesha kitu katika ulimwengu. Wanatambua kuwa hayo ni ya Allaah. Wanasema kuwa ni wakati kati na waombezi wao. Kuna wenye kusema watu sampuli hii ni waislamu. Tunawauliza ni kwa nini makafiri wa ki-Quraysh na wao pia wasiwe waislamu? Mwenye kusema hivi hana uelewa na ujuzi wa Tawhiyd kwa kuwa hakuielewa Tawhiyd.

Ni wajibu kwa mtu atambue jambo hili kwa kuwa ni muhimu sana. Huu ndio utamaduni sahihi. Utamaduni sio kutambua hali za ulimwengu, serikali na siasa mbalimbali. Huu ni utamaduni usionufaisha wala kudhuru. Utamaduni wenye kunufaisha ni kule kutambua Tawhiyd sahihi na kutambua vilevile ile shirki inayopingana nayo au Bid´ah na mambo ya uzushi inayoipunguza. Huu ndio utamaduni sahihi na haya ndio wajibu kwa muislamu na kwa mwanafunzi aitambue Tawhiyd na alinganie kwayo. Hili ndilo linatakikana. Elimu nyingi inanufaisha nini pasi na uhakiki na uoni? Haunufaishi wala haumfidishii yule mwenye nayo kitu ikiwa haikujengwa juu ya uhakiki na Tawhiyd na kumuabudu Allaah na kuitambua haki kutokamana na batili. Hayamnufaishi mwenye nayo kitu ikiwa ni kusoma tu au utamaduni tu wa kijumla.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Kashf-ish-Shubuhaat, uk. 24-25
  • Imechapishwa: 15/10/2016