16. Mkate na maji kwa ajili ya kuelekea Peponi

68 – Surayj ametuhadithia: Yaziyd bin Haaruun ametuhadithia: al-Mas´uudiy ametukhabarisha, kutoka kwa ´Aliy bin Badhiymah, kutoka kwa Abu ´Ubaydah, ambaye amesema:

”Wafuasi walimwambia ´Iysaa mwana wa Maryam (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam): ”Tutakula nini?” Akasema: ”Mkate wa shayiri.” Wakasema: ”Tutakunywa nini?” Akasema: ”Maji masafi.” Wakasema: ”Tutalalia kitu gani?” Akasema: ”Juu ya ardhi.” Wakasema: ”Hakuna kingine unachotuamrisha isipokuwa maisha magumu.” Akasema: ”Hivo ndio unafikiwa ufalme wa mbinguni, ili asiwepo yeyote katika nyinyi atakayeyaendea matamanio yake.” Wakasema: ”Inakuweje?” Ndipo akasema: ”Hujaona jinsi mtu mwenye njaa hakuna anachokipenda zaidi kama kipande cha mkate, jinsi anavyokuwa na kiu anavyoyapenda zaidi maji, hata kama yatakuwa masafi, na jinsi ambavyo aliyesimama kwa muda mrefu anavyopenda zaidi kulala juu ya ardhi?”

69 – ´Abdur-Rahmaan bin Waaqid na wengineo wametuhadithia: Khalaf bin Khaliyfah wametuhadithia, kutoka kwa Humayd al-A´raj, kutoka kwa ´Abdullaah bin al-Haarith, kutoka kwa ´Aliy, ambaye amesema:

”Mashimo mawili yamemwangamiza mwanadamu: tumbo na tupu.”

70 – Muhammad bin Idriys amenihadithia: ´Amr bin Aslam ametuhadithia: Nimemsikia Salm bin Maymuun al-Khawwaas akisema:

Vovyote vile utakavyoliridhisha tumbo na tupu yako

ukweli wa mambo ndio lawama ya mwisho kabisa

71 – ´Abdur-Rahmaan bin Swaalih al-´Atakiy ametuhadithia: ´Abdullaah bin al-Muttwalib al-´Ijliy ametuhadithia, kutoka kwa al-Hasan bin Dhakwaan, kutoka kwa Yahyaa bin Abiy Kathiyr, kutoka kwa Abu Salamah, kutoka kwa Abu Hurayrah, kutoka kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), ambaye amesea:

”Chakula kinapokuwa kichache kwa watu wa nyumbani, basi nyumba zao zinang´aa.”[1]

[1] Imezuliwa kwa mujibuwa Ibn-ul-Jawziy katika “al-Mawdhuw´aat” (3/35), ash-Shawkaaniy katika “al-Fawaa-id al-Majmuw´ah”, uk. 157, na al-Albaaniy katika “adh-Dhwa´iyfah” (166).

  • Mhusika: Imaam Abu Bakr ´Abdullaah bin Muhammad bin Abiyd-Dunyaa
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-ul-Juu´, uk. 65-67
  • Imechapishwa: 19/06/2023