62 – Khaalid bin Khidaash ametuhadithia: al-Mu´allaa bin al-Warraaq ametuhadithia: Nilimsikia Abu ´Ubaydah al-Khawwaas akisema:

”Mtu mwenye khasara zaidi ni yule mwenye kuingia Motoni kwa sababu ya wengine. Tumbo lako ndio mbwa wako. Kwa hivyo mkimbize mbali kwa tonge.”

63 – Muhammad bin ´Aliy al-Muqaddimiy amenihadithia: Nilimsikia Yuusuf bin ´Atwiyyah bin Baab: Nilimsikia Maalik bin Diynaar akisema:

”Naapa kwa Allaah! Natamani ningenyonya mawe, na hivyo nikaweza kuishi kwayo, yakanitosheleza kutokamana na chakula na kinywaji.”

64 – Ishaaq bin Ibraahiym ametuhadithia: Wakiy´ ametuhadithia, kutoka kwa ´Abdul-Waahid bin Zayd, kutoka kwa al-Hasan, ambaye amesema:

”Nilikutana na watu wanaotamani kile chakula wanachokula matumboni mwao kingekuwa ni mawe.”

65 – Ibraahiym bin ´Abdillaah al-Harawiy ametuhadithia: Ja´far bin Sulaymaan ametukhabarisha: Nilimsikia Maalik bin Diynaar akisema:

”Hakika matumbo yenu ni mijibwa yenu. Tupa ndani yake kipande cha mkate na kijisamaki, ili iache kukubwekea. Msiyafanye matumbo yenu ni vifuko vya shaytwaan ambamo Ibliys anakihifadhi anachokitaka.”

66 – Muhammad bin ´Aliy al-Muqaddimiy amenihadithia: Ndugu yangu ´Ubaydullaah amenihadithia: Maalik bin Diynaar amesema:

”Hakuna kati yetu sisi na Hishaam bin ´Abdil-Malik isipokuwa kukishinda hiki kisha [tupu] unampendelea. Bi maana [tupu].”

67 – Surayj ametuhadithia, kutoka kwa Yuunus: Rawh bin ´Ibaadah ametuhadithia: Hishaam ametuhadithia, kutoka kwa al-Hasan ambaye amesema:

”Naapa kwa Allaah! Tumekutana na watu, kutangamana na wengi, ambao hakuna hata siku moja mmoja katika wao aliyewaamrisha familia yake kuwapikia chakula. Hakuna yeyote katika wao aliyekula akashiba mpaka walipokufa. Mara tu walipokaribia kushiba, walijizuia na kula.”

  • Mhusika: Imaam Abu Bakr ´Abdullaah bin Muhammad bin Abiyd-Dunyaa
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-ul-Juu´, uk. 63-65
  • Imechapishwa: 19/06/2023