14. Mara kushiba, mara kuwa na njaa

59 – Surayj ametuhadithia: Hushaym ametuhadithia: Mansuur  ametukhabarisha, kutoka kwa Ibn Siyriyn, ambaye ameeleza:

”Bwana mmoja alikuja kwa Ibn ´Umar akasema: ”Tusikupikie uji wa ngano?” Akasema: ”Na ni kitu gani huo uji wa ngano?” Akasema: ”Ni kitu ambacho hulainisha hisia zako za shibe unapokuwa umekula na ukashiba.” Ndipo Ibn ´Umar akasema: ”Sijashiba tangu miezi minne iliyopita. Na si kwamba eti sikipati, lakini nina uzoefu wa watu ambao wakati fulani wanahisi njaa na wakati mwingine wanashiba.”

60 – Ishaaq bin Ismaa´iyl ametuhadithia: Abu Mu´aawiyah ametuhadithia, kutoka kwa al-A´mash, kutoka kwa Naafiy´, ambaye amesema:

”Wakati ambapo Ibn ´Umar aliugua, Swafiyyah akamtumia kijakazi kumnunulia rundo la sarafu ya fedha. Mwombaji akamuona akamfuata. Wakati kijakazi alipoingia ndani, akasema: ”Masikini! Masikini!” Ibn ´Umar akasema: ”Mpe nayo. Mpe nayo.” Ndipo Swafiyyah akamtuma kijakazi yule kwa sarafu nyingine ya fedha ambapo akamnunulia rundo lingine. Mwombaji akamuona akamfuata. Wakati kijakazi alipoingia ndani, akasema: ”Masikini! Masikini!” Ibn ´Umar akasema: ”Mpe nayo.” Kisha mara ya tatu akamtuma kwa sarafu nyingine ya fedha na akasema: ”Naapa kwa Allaah! Ukirudi basi kamwe sintokupa kingine tena!” Akaacha. Hivyo akamnunulia rundo.”

61 – Khaalid bin Khidaash ametuhadithia: Mahdiy bin Maymuun ametuhadithia, kutoka kwa Muhammad bin Siyriyn, ambaye ameeleza:

”Ilikuwa inaweza kutokea wakati mwingine mtu katika Maswahabah wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) inampitikia siku tatu pasi na kupata kitu cha kukula. Hatimaye alikuwa anaweza kuchukua ngozi akaichoma na kuila. Asipopata kitu kabisa, basi anachukua jiwe na kulifunga kwenye mwili wake ili unyooke uti wa mgongo wake.”

  • Mhusika: Imaam Abu Bakr ´Abdullaah bin Muhammad bin Abiyd-Dunyaa
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-ul-Juu´, uk. 61-62
  • Imechapishwa: 19/06/2023