16. Hadiyth ”Liguse mchanga pua la yule ambaye nitatajwa mbele yake… “

16 – Musaddad ametuhadithia: Bishr bin al-Mufadhdhwal ametuhadithia: ´Abdur-Rahmaan bin Ishaaq ametuhadithia, kutoka kwa Sa´iyd al-Maqburiy, kutoka kwa Abu Hurayrah, ambaye ameeleza kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

رغم أنف رجل ذكرت عنده فلم يصلِّ علي، ورغم أنف رجل أدرك أبويه عند الكبر فلم يدخلاه الجنة، ورغم أنف رجل دخل عليه رمضان، ثم انسلخ قبل أن يغفر له

”Liguse mchanga pua la yule ambaye nitatajwa mbele yake na asiniswalie. Liguse mchanga pua la yule ambaye amekutana na wazazi wake wakati wa uzee wao na wasimwingize Peponi. Liguse mchanga pua la yule ambaye atafikiwa na Ramadhaan kisha ikamalizika kabla ya yeye kusamehewa.”[1]

17 – al-Maqdamiy ametuhadithia: Yaziyd bin Zuray´ ametuhadithia: ´Abdur-Rahmaan bin Ishaaq ametuhadithia mfano wake…

[1] Cheni ya wapokezi wake ni Swahiyh. Wanamme wake ni wanamme Swahiyh. Ameipokea at-Tirmidhiy na al-Haakim. Sentesi ya pili iko kwa Muslim. Ibn Hibbaan (2387) ameipokea kupitia njia nyingine kwa toleo kamilifu zaidi kwa cheni ya wapokezi nzuri.

  • Mhusika: Imaam Ismaa´iyl bin Ishaaq al-Maalikiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fadhwl-us-Swalaah ´alaan-Nabiy, uk. 3
  • Imechapishwa: 03/01/2024
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy