15. Hadiyth ”Liguse mchanga pua la yule ambaye utatajwa mbele yake na asikuswalie… “

15 – ´Abdullaah bin Maslamah ametuhadithia: Salamah bin Wardaan ametuhadithia: Nimemsikia Anas bin Maalik akisema:

حدثنا عبد الله بن مسلمة، قال ثنا سلمة بن وردان، قال سمعت أنس بن مالك يقول:  ارتقى النبي صلى الله عليه وسلم على المنبر درجة فقال: آمين، ثم ارتقى الثانية فقال: آمين، ثم ارتقى الثالثة فقال: آمين، ثم استوى فجلس، فقال أصحابه: على ما أمَّنت؟ قال

أتاني جبريل فقال: رغم أنف امرئ ذكرتَ عنده فلم يصلِّ عليك، فقلت آمين، فقال: رغم أنف امرئ أدرك أبويه فلم يدخل الجنة، فقلت: آمين، فقال: رغم أنف امرئ أدرك رمضان فلم يغفر له، فقلت آمين

”Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipanda juu ya mimbari ngazi moja akasema: ”Aamiyn.” Kisha akapanda ngazi ya pili akasema: ”Aamiyn.” Kisha akapanda ngazi ya tatu akasema: ”Aamiyn.” Alipofika juu akaketi chini. Maswahabah wakasema: ”Kwa nini umesema ´Aamiyn`?” Akasema: ”Nimejiliwa na Jibriyl akasema: ”Liguse mchanga pua la yule ambaye utatajwa mbele yake na asikuswalie.” Nikasema: ”Aamiyn.” Akasema: ”Liguse mchanga pua la yule ambaye amekutana na wazazi wake na asiingie Peponi.” Nikasema: ”Aamiyn.” Akasema: ”Liguse mchanga pua la yule ambaye atakutana na Ramadhaan na asisamehewe!” Nikasema: ”Aamiyn.”[1]

[1] Hadiyth ni Swahiyh kupitia Hadiyth nyenginezo zinazokuja huko mbele zinazoitia nguvu. Ibn Maasiy ameipokea katika “al-Fawaaid” (09/01-02) na kwa tamko lililotangulia (04).

  • Mhusika: Imaam Ismaa´iyl bin Ishaaq al-Maalikiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fadhwl-us-Swalaah ´alaan-Nabiy, uk. 32
  • Imechapishwa: 03/01/2024
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy