14. Hadiyth ”Kutakuja chenye kutetemesha, kifuatiwe na cha pili yake… “

14 – Sa´iyd bin Salaam al-´Attwaar ametuhadithia: Sufyaan (ath-Thawriy) ametuhadithia, kutoka kwa ´Abdullaah bin Muhammad bin ´Aqiyl, kutoka kwa at-Twufayl bin Abiy Ka´b, kutoka kwa baba yake, ambaye amesema:

كان رسول الله صلى الله عليه وسلم يخرج في ثلثي الليل فيقول: جاءت الراجفة تتبعها الرادفة، جاء الموت بما فيه، وقال أبَيّ؟؟: يا رسول الله إني أصلي من الليل: أفأجعل لك ثلث صلاتي؟ قال رسول الله صلى الله عليه وسلم (الشطر) .

قال: أفأجعل لك شطر صلاتي؟ قال رسول الله صلى الله عليه وسلم (الثلثان أكثر)

قال: أفأجعل لك صلاتي كلها؟ [قال:])

(إذن يغفر لك ذنبك كله)

”Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akitoka katika theluthi ya usiku akisema: ”Kutakuja chenye kutetemesha, kifuatiwe na cha pili yake. Kifo na yale yote yenye maana yake.” Ubayy akasema: “Ee Mtume wa Allaah! Hakika naswali swalah za usiku; nisikufanyie theluthi ya du´aa yangu?” Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasema: ”Nusu yake.” Akasema: ”Nisikufanyie nusu ya du´aa yangu?” Akasema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam): ”Thuluthi mbili ni nyingi.” Akasema: ”Nisikufanyie du´aa[1] yangu yote?” Ndipo akasema: ”Basi hapo utasamehewa dhambi zako zote.”[2]

[1] Hapa swalah kunakusudiwa du´aa, kama unavyofahamisha upokezi uliotangulia.

[2] Hadiyth ni nzuri. Upokezi wa al-´Attwaar sio wa kufurahia, lakini imesimuliwa pia na Qabiyswah, kutoka kwa Sufyaan. Hadiyth hii ameipokea at-Tirmidhiy na akasema kuwa ni nzuri na Swahiyh.

  • Mhusika: Imaam Ismaa´iyl bin Ishaaq al-Maalikiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fadhwl-us-Swalaah ´alaan-Nabiy, uk. 31-32
  • Imechapishwa: 03/01/2024
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy