Mpaka hapa tunamalizia kuzungumzia masharti yanayopaswa kutimizwa na vazi na jilbaab ya mwanamke. Mukhtaswari wake ni kama ifuatavyo:

1 – Ni wajibu kwake kufunika mwili wake wote isipokuwa uso na mikono yake, kwa upambanuzi uliyotangulia.

2 – Jilbaab yenyewe kama yenyewe isiwe ni pambo.

3 – Jilbaab isiwe yenye kuonyesha ndani.

4 – Jilbaab isiwe yenye kubana kwa njia ya kuwa inaonyesha maumbo ya mwili wake.

5 – Jilbaab isiwe ni yenye kutiwa manukato.

6 – Jilbaab isiwe ni yenye kufanana na mavazi ya wanaume na mavazi ya makafiri.

7 – Jilbaab isiwe ni vazi lenye kufanya watu kukataka kumtazama na kujulikana.

Ni wajibu kwa kila muislamu kuhakikisha masharti yote haya yametimia kwa mke wake na kila ambaye yuko chini ya usimamizi wake, kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Nyote ni wachungaji na kila mmoja ataulizwa kwa kile alichokichunga. Kiongozi ni mchungaji na ataulizwa kwa kile alichokichunga. Mwanaume ni mchungaji wa familia yake na yeye ataulizwa kwa kile alichokichunga. Mwanamke ni mchungaji na yeye ataulizwa juu ya nyumba ya mume wake.”[1]

Allaah (´Azza wa Jall) amesema:

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا قُوا أَنفُسَكُمْ وَأَهْلِيكُمْ نَارًا وَقُودُهَا النَّاسُ وَالْحِجَارَةُ عَلَيْهَا مَلَائِكَةٌ غِلَاظٌ شِدَادٌ لَّا يَعْصُونَ اللَّـهَ مَا أَمَرَهُمْ وَيَفْعَلُونَ مَا يُؤْمَرُونَ

“Enyi mlioamini! Jikingeni nafsi zenu na familia zenu na Moto ambao mafutayake ni watu na mawe; juu yake wako Malaika wakali, shadidi hawamuasi Allaah kwa yale anayowaamrisha na wanafanya yale wanayoamrishwa.”[2]

Namuomba Allaah (Ta´ala) atuwafikishe katika kufuata amri Zake na kuepuka makatazo Yake:

سُبْحانَكَ اللهُمَّ وَبِحَمْدِكَ أَشْهَدُ أَنْ لا إِله إِلا أَنْتَ أَسْتَغْفِرُكَ وَأَتُوبُ إِلَيْكَ

Kutakasika kutokamana na mapungufu na himdi zote ni Zako, ee Allaah. Nashuhudia ya kwamba hapana mwabudiwa wa haki isipokuwa Wewe. Nakuomba msamaha na nakutubia Kwako.

Imeandikwa na

Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy

Abu ´Abdir-Rahmaan

1371-05-09

Dameski

[1] al-Bukhaariy (7138) na Muslim (1829).

[2] 66:6

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Jilbaab-ul-Mar-ah al-Muslimah, uk. 211
  • Imechapishwa: 28/11/2023