“Watu wa nchi fulani wana tabia kadhaa”

Swali: Baadhi ya watu wanaisema vibaya baadhi ya miji. Je, inazingatiwa ni usengenyi?

Jibu: Usengenyi ni kumsema vibaya mtu maalum. Kusema kwa ujumla sio usengenyi.

Swali: Kwa mfano wakisema nchi fulani…

Jibu: Kusema kuwa baadhi ya watu wanafanya kadhaa na baadhi ya watu wa mji fulani wanafanya hivi. Huku sio kusengenya. Isipokuwa akisema fulani mwana wa fulani. Ninachotaka kusema ni kwamba asipotaja jina sio usengenyi. Kutaja mji fulani haidhuru.

Swali: Wanawatia aibu watu wa nchi fulani?

Jibu: Kutaja nchi haiwi usengenyi. Usengenyi ni pale anapomtaja mtu kwa dhati yake.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23214/هل-من-الغيبة-التنكيت-على-بعض-البلدان
  • Imechapishwa: 28/11/2023