153. Jilbaab haifai ikawa yenye kushuhurika

Sharti ya nane ya jilbaab ni kwamba lisiwe ni vazi lenye kufanya watu kutaka kumtazama na kutambulika[1]. Ibn ´Umar (Radhiya Allaahu ´anhumaa) amesimulia kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Yule ambaye atavaa vazi la kutaka watu wamtambue duniani, basi Allaah atamvisha vazi la udhalilifu siku ya Qiyaamah. Kisha atayawashia moto.”[2]

[1] Na kila nguo ambayo malengo ni kutaka kutazamwa na kutambulika kati ya watu, ni mamoja nguo hiyo ni ya thamani ambayo mtu ameivaa kwa ajili ya kutaka fakhari duniani na mapambo yake, au la kudharauliwa ambalo amelivaa kwa ajili ya kuonyesha kuwa ni mwenye kuipa nyongo duniani na kutaka kujionyesha. ash-Shawkaaniy amesema:

”Kutaka kutazamwa na kutambulika (الشهرة) ni kukionyesha kitu. Katika hali hii kinachokusudiwa ni kuwa nguo yake inatofautiana na nguo za wengine ambapo watu wakamnyanyulia macho yao. Akajigamba mbele yao, kwa kujiona na mwenye kiburi.” (Nayl-ul-Awtwaar (2/94))

[2] Abu Daawuud na Ibn Maajah kupitia kwa Abu ´Awaanah, kutoka kwa ´Uthmaan bin al-Mughiyrah, kutoka kwa al-Muhaajir, kutoka kwa Ibn ´Umar.

Cheni yake ya wapokezi ni nzuri, ndivo alivosema Ibn-ul-Mundhir katika ”at-Targhiyb wat-Tarhiyb” (3/112). Wasimulizi wa cheni yake ya wapokezi ni wenye kuaminika, kama alivosema ash-Shawkaaniy.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Jilbaab-ul-Mar-ah al-Muslimah, uk. 213
  • Imechapishwa: 28/11/2023