Kwa ajili hiyo tunamuona Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akikataza kutofautiana hata mahali watu wamekaa. Hivi sasa nahudhurikiwa na Hadiyth mbili:

1 – Jaabir bin Samurah amesema:

”Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alitutokea na akatuona tumekaa makundimakundi. Akasema: ”Ni kwa nini nakuoneni mmetengana?”[1]

2 – Tha´labah al-Khushaniy (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:

”Watu walipokuwa wanapiga kambi, basi wanatawanyika katika njia za milima na mabonde. Ndipo Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasema: ”Hakika kutawanyika kwenu katika njia hizi za milima na mabonde kunatokana na shaytwaan.” Kuanzia wakati huo hawakupiga kambi yoyote isipokuwa walikuwa wakisogeleana. Mpaka mtu alikuwa anaweza kusema lau kitambaa kingetandazwa kwao, basi kingeliwafunika wote.”[2]

[1] Muslim, Ahmad na at-Twabaraaniy katika ”al-Mu´jam al-Kabiyr”.

Hadiyth inakataza kufarikiana na inaamrisha kuwa wamoja, hivo ndivo alivosema an-Nawawiy katika ”Sharh Swahiyh Muslim”.

[2] Abu Daawuud, Ibn Hibbaan, al-Haakim, kupitia kwake al-Bayhaqiy na Ahmad kupitia kwa al-Waliyd bin Muslim: ´Abdullaah bin Zabr ametuhadithia kuwa amemsikia Muslim bin Mishkam akisema: Abu Tha´labah al-Khushaniy ametuhadithia.

Cheni hii ya wapokezi ni Swahiyh na yenye kuungana. al-Haakim amesema:

”Cheni ya wapokezi ni Swahiyh.”

adh-Dhahabiy ameafikiana naye.

Zabr ni baba yake na ´Abdullaah. Baba yake jina lake anaitwa al-´Alaa´.

Kidokezo! Ikiwa kufarikiana huku katika jambo la kawaida kunatokana na kitendo cha shaytwaan, tuseme nini kuhusu kutofautiana katika mambo ya dini na katika nguzo yake kubwa zaidi ya kimatendo kama vile swalah? Hii leo tunawaona jinsi waislamu wanatofautiana katika swalah zao nyuma ya maimamu mbalimbali kwenye msikiti mmoja. Je, jambo hilo halitokamani na shaytwaan? Ndio, naapa kwa Mola wangu! Lakini wengi hawajui.

إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَذِكْرَىٰ لِمَن كَانَ لَهُ قَلْبٌ أَوْ أَلْقَى السَّمْعَ وَهُوَ شَهِيدٌ

“Hakika katika hayo bila shaka ni ukumbusho kwa mwenye moyo au akatega sikio naye mwenyewe awe hadhiri.” (50:37)

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Jilbaab-ul-Mar-ah al-Muslimah, uk. 210-212
  • Imechapishwa: 28/11/2023