Kwa hivyo ikafahamisha kujitofautisha na makafiri na kuacha kujifananisha nao ni miongoni mwa malengo makubwa makubwa ya ki-Shari´ah. Ni wajibu kwa waislamu wote wanaume na wanawake walitilie umuhimu jambo hilo, khaswa inapokuja katika mavazi na nguo zao, kama ilivyothibitishwa katika dalili maalum. Kwa hiyo imethibiti dalili ya nane juu ya vazi la mwanamke.

Wanaweza kufikiria baadhi ya watu kwamba kujitofautisha kunakozungumziwa ni jambo la ki-´ibaadah peke yake. Mambo sivyo. Ni jambo pia linaloingia akilini na hekima yake iko wazi. Wanazuoni wahakiki wamethibitisha kuwa kuna mafungamano yenye nguvu kati ya uinje na undani, na kwamba uinje una athari yenye nguvu juu ya yale ya ndani. Ikiwa nzuri, inakuwa nzuri, na ikiwa ni mbaya, inakuwa mbaya. Ingawa huenda ikawa ni jambo ambalo mtu mwenyewe asiweze kulihisi, hata hivyo anaweza kuliona kwa wengine. Shaykh-ul-Islaam (Rahimahu Allaah) amesema:

”Hili ni jambo linaloshuhudiwa na hisia na uzoefu. Watu wawili wanaotokea mji mmoja ambao wanakutana katika nchi ya kigeni, kunakuwa kati yao na mapenzi makubwa na kuungana ijapo katika mji wao hawakuwa wenye kujuana, au pengine hata walikuwa sio marafiki. Hilo ni kwa sababu ule ushirikiano wao unawafanya kushirikiana katika nchi ya kigeni. Bali endapo watu watakuwa na vilemba, nguo, staili za nywele au vipando vya kufanana, basi wanakuwa na ukaribu na kuungana zaidi kuliko wengine. Unaweza kuona jinsi watu wa taaluma fulani wanavyoelewana zaidi kuliko wanavyoshirikiana na vikundi vingine vya taaluma. Uzoefu huo unaweza kutokea hata kati ya watu ambao wako na uadui kati yao, ima unaohusiana na utawala au dini. Utawaona wafalme na viongozi, ijapo nchi zao zitakuwa mbalimbali, wanahisi kuungana na kufanana wao kwa wao. Haya yote ndivo yanavopelekea maumbile na yote yenye maana yake. Kitu pekee kinachoweza kuzuia jambo hilo ni dini au lengo maalum.

Ikiwa kujifananisha katika mambo ya kidunia kunapelekea katika mapenzi, kusemwe nini juu ya kujifananisha katika mambo ya kidini? Kujifananisha kama huko ni kubaya na mapenzi makubwa zaidi. Kuwapenda kunapingana na imani… Allaah (Subhaanah) amesema:

لَّا تَجِدُ قَوْمًا يُؤْمِنُونَ بِاللَّـهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ يُوَادُّونَ مَنْ حَادَّ اللَّـهَ وَرَسُولَهُ وَلَوْ كَانُوا آبَاءَهُمْ أَوْ أَبْنَاءَهُمْ أَوْ إِخْوَانَهُمْ أَوْ عَشِيرَتَهُمْ ۚ أُولَـٰئِكَ كَتَبَ فِي قُلُوبِهِمُ الْإِيمَانَ وَأَيَّدَهُم بِرُوحٍ مِّنْهُ

“Hutopata watu wanaomuamini Allaah na siku ya Mwisho kuwa wanawapenda wale wanaopinzana na Allaah na Mtume Wake, japo wakiwa ni baba zao, watoto wao, ndugu zao au jamaa zao. Hao [Allaah] amewaandikia katika nyoyo zao imani na akawatia nguvu kwa Roho kutoka Kwake.”[1]

Akakhabarisha (Subhaanahu wa Ta´ala) ya kwamba hutompata muumini anayempenda kafiri, na kwamba anayewapenda makafiri sio muumini. Muda wa kuwa kujifananisha kunapelekea katika mapenzi, ni haramu.”[2]

[1] 58:22

[2] Iqtidhwaa’-us-Swiraat al-Mustaqiym, uk. 105-106

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Jilbaab-ul-Mar-ah al-Muslimah, uk. 206-207
  • Imechapishwa: 28/11/2023